Afya

Okoka maisha na saidia kupunguza kasi ya kuenea kwa virusi vya corona nchini Australia

KAA NYUMBANI

 • Usiondoke nyumbani isipokuwa unapaswa kufanya.
 • Unapaswa kuepuka kuondoka nyumba yako kwa shughuli zozote zisizo lazima.
 • Usikaribishe wanafamilia au marafiki kuingia nyumba yako.
 • Kaa nyumbani isipokuwa unafanya ifuatayo:
  • kwenda kazini au elimu (ikiwa huwezi kufanya hivyo nyumbani)
  • kununua mahitaji kama chakula (rudi nyumbani bila kuchelewa)
  • kwenda nje kwa mazoezi ya kibinafsi katika ujirani, peke yako au pamoja na mtu mwingine
  • kwenda miadi ya kimatibabu au kutembelea kwenye huruma.
 • Huduma za kimatibabu, maduka makubwa, benki, vituo vya mafuta, huduma za posta na kuleta vitu nyumbani zinaendelea wazi.

JITUNZE USALAMA

 • Wakati wote fanya usafi mzuri, osha mikono yako kwa sekondi 20 kukitumia sabuni na maji, funika kohozi yako, epuka kugusa macho yako, pua na mdomo wako.
 • Endelea kujiweka umbali wa anglau wa mita 1.5 wakati yupo nje ya nyumbani.
 • Epuka salamu ya kimwili kama kushikana mikono, kumbatia na busu.
 • Tumia kadi kugonga na kulipa badala ya fedha taslimu.
 • Usafiri wakati wa tulivu na epuka makundi ya watu.
 • Jua vema – tumia pekee habari rasmi zilizoaminifu. Pakua app ya Coronavirus Australia ya simu ya mkononi, ujiunge huduma ya Coronavirus Australia WhatsApp, na tembelea www.australia.gov.au kwa habari za kisasa.

ENDELEA KUHUSIANA

 • Chunguza hali ya wanafamilia na marafiki kwa simu au mtandaoni.
 • Leta chakula na vitu vya muhimu kwa jamaa wakubwa, wazee na watu wenye udhaifu. Uache vitu vile mlangoni tu.
 • Mashirika makuu ya kujitolea na ya kusaidia wenye shida bado yataweza kutoa huduma kwa wale ambao wanahitaji zile zaidi.

Habari za afya

Dalili za virusi vya corona ni pamoja na:

 • homa
 • kikohozi
 • koo yenye maumivu
 • uchovu
 • upungufu wa pumzi

Ikiwa wewe ni mgonjwa na unafikiri unaweza kuwa na virusi vya corona, upate msaada wa kimatibabu.

Unaweza kupiga simu Laini ya Kitaifa cha Msaada wa virusi vya Corona ili kupata habari. Ikiwa unahitaji huduma za utafsiri au ukalimani, pigia simu kwenye 131 450.

Ikiwa una dalili kubwa kama ugumu wa kupumua, piga simu 000 ili kupata msaada wenye dharua wa kimatibabu.

Tovuti ya Idara ya Afya ina habari mbalimbali inayopatikana katika lugha badala ya Kiingereza ili kusaidia watu kuwa salama na kupunguza hatari kwa jamii.