Biashara

Nyongeza ya JobKeeper

Malipo ya JobKeeper, ambayo yalitokana mwanzoni hadi tarehe ya 27 Septemba 2020, itaendelea kupatikana kwa biashara zinazostahiki (pamoja na wanaojiajiri) na mashirika ya sio kwa faida hadi tarehe ya 28 Machi 2021.

Kwa muhtasari wa mabadiliko yanayokuja tafadhali angalia treasury.gov.au/coronavirus/jobkeeper/extension.

Malipo ya JobKeeper

Malipo ya JobKeeper ya Serikali ni ruzuku ya muda kwa biashara zilizoathiriwa sana na virusi vya korona (COVID-19).

Waajiri, wafanyabiashara wa pekee na vyombo vingine wanaostahiki wanaweza kuomba kupokea malipo ya JobKeeper kwa wafanyakazi wao wanaostahili. Hii italipwa kwa mwajiri kwa kiporo kwa kila mwezi na ATO.

Biashara zinaweza kujiandikisha kwa Malipo ya JobKeeper kupitia Lango la Biashara (Business Portal ya ATO, katika huduma za mtandaoni za ATO (ATO online services), kwa kutumia MyGov ikiwa wewe ni mfanyabiashara pekee, au kupitia wakala aliyesajiliwa wa kodi au BAS.

Kwa habari juu ya msaada uliopo wa JobKeeper na msaada kutoka ATO nenda kwa www.ato.gov.au/JobKeeper

Kuhakikisha mapato halisi kulipia bili na mishahara

Biashara zinazostahiki na mashirika yasiyo ya faida (NFP) ambayo zinajiri wafanyakazi watapokea kati ya $20,000 hadi $100,000 kwa kiasi kuongeza mapato halisi kwa kuweka taarifa zao za shughuli hadi mwezi au robo mwaka ya Septemba 2020.

Jifunze zaidi:

Wanagenzi na wakurufunzi

Serikali inaunga mkono maendeleo endelevu ya wafanyakazi wenye ustadi wa Australia na kusaidia biashara zinazostahili kuendelea kuajiri wanagenzi na wakurufunzi kwa kutoa ruzuku ya mshahara wa asilimia ya 50 hadi $21,000.

Jifunze zaidi:

Madeni na mikopo

Mpango mpya wa Dhamana ya virusi vya corona SME unamaanisha kuwa unaweza kupata mikopo ya ziada kutoka wakopeshaji wanaoshiriki kukuunga mkono kupitia miezi ijayo.

Serikali itatoa dhamana ya asilimia 50 kwa wakopeshaji wa SME kwa mikopo mipya isiyolindwa itumike kwa mtaji wa kufanya kazi.

Serikali pia inatoa msamaha kutoka majukumu ya kukopesha uwajibikaji kwa wakopeshaji kutoa mikopo kwa wateja waliopo wa biashara ndogo.

Msamaha huu ni muda wa miezi sita na inatumika kwa madeni yoyote kwa madhumuni ya biashara, pamoja na mkopo mpya, ongezeko la kikomo cha mkopo na mabadiliko na marekebisho ya mkopo.

Kusaidia mikoa na sekta

Serikali imeweka kando $1 bilioni kusaidia jamii, mikoa na viwanda vilivyoathiriwa sana na mlipuko wa virus vya corona. Fedha hizi zitapatikana kusaidia wakati wa mlipuko na kusaidia na upatikanaji tena. Kwa kuongezea, Serikali inasaidia tasnia yetu ya ndege kupitia kifurushi cha hadi $715 milioni.

Kuwekeza katika biashara yako

Kizingiti cha uondoaji wa mali ya papo hapo kimeongezwa kutoka $30,000 hadi $150,000 kwa biashara na mauzo ya jumla ya mwaka chini ya $500 milioni.

Ikiwa unanunua vifaa vipya kwa ghala yako au trekta iliyokwishatumiwa, biashara yako inaweza kufaidika kutokana na kuongezeka na kupanuka kwa uondoaji wa mali ya papo hapo hadi 31 Desemba 2020. 

Vipunguzi vya uchakavu vya kasi pia vitapatikana kwa biashara inayostahili kupitia mpango wa kishawishi wa uwekezaji wa miezi 15.

Jifunze zaidi:

Instant asset write-off for eligible businesses (Kufuta mali ya mara moja kwa biashara inayostahili

Backing business investment – accelerated depreciation (Kuunga mkono uwekezaji – upunguzaji thamani)

Angalia pia: