Chanjo za COVID-19

Tunahimiza kila mtu anayeishi katika jamii ya Australia kupata chanjo. Hii inaendana na ushauri wa kiafya.

Chanjo za COVID-19 ni bure kwa kila mtu nchini Australia, ikiwa ni pamoja na:

  • wamiliki wa viza ya Australia
  • wageni wa nje ya nchi
  • wanafunzi wa kimataifa
  • wafanyakazi wahamiaji
  • watafuataji wa hifadhi, na
  • watu ambao hawana viza halali.

Wakati watu nchini Australia wanapopata chanjo, habari juu ya hali yao ya uhamiaji au uraia haikusanyikwi.

Huna haja ya kustahiki au kujiandikishwa kwa Medicare ili kupokea chanjo bure ya COVID-19. Ili kupata kliniki ambapo huna haja ya kadi ya Medicare, tumia COVID-19 Vaccine Eligibility Checker.

Kwa maelezo zaidi juu ya mpango wa chanjo ya COVID-19 katika lugha yako, tembelea COVID-19 vaccine information in your language.