Kwa Biashara

Malipo ya JobKeeper

Malipo ya JobKeeper ya Serikali yalikuwa ruzuku ya muda kwa biashara zilizoathiriwa sana na virusi vya korona (COVID-19).

Waajiri, wafanyabiashara wa pekee na vyombo vingine wanaostahiki wangeweza kuomba kupokea malipo ya JobKeeper kwa wafanyakazi wao wanaostahili. Hii ililipwa kwa mwajiri kwa kiporo kwa kila mwezi na ATO.

Biashara zinaweza kujiandikisha kwa Malipo ya JobKeeper kupitia Lango la Biashara (Business Portal ya ATO, katika huduma za mtandaoni za ATO (ATO online services), kwa kutumia MyGov ikiwa walikuwa wafanyabiashara pekee, au kupitia wakala aliyesajiliwa wa kodi au BAS.

Kwa habari juu ya Malipo ya JobKeeper nenda kwa www.ato.gov.au/JobKeeper

Kuhakikisha mapato halisi kulipia bili na mishahara

Biashara zinazostahiki na mashirika yasiyo ya faida (NFP) ambayo zinajiri wafanyakazi watapokea kati ya $20,000 hadi $100,000 kwa kiasi kuongeza mapato halisi kwa kuweka taarifa zao za shughuli za kila mwezi na za kila mwaka robo kutoka Machi 2020 hadi mwezi ya Septemba 2020.

Jifunze zaidi:

Wanagenzi na wakurufunzi

Serikali inaunga mkono maendeleo endelevu ya wafanyakazi wenye ustadi wa Australia na kusaidia biashara zinazostahili kuendelea kuajiri wanagenzi na wakurufunzi kwa kutoa ruzuku ya mshahara wa asilimia ya 50 hadi $21,000.

Jifunze zaidi:

Madeni na mikopo

Mpango mpya wa Dhamana ya virusi vya corona SME unamaanisha kuwa unaweza kupata mikopo ya ziada kutoka wakopeshaji wanaoshiriki kukuunga mkono kupitia miezi ijayo.

Serikali itatoa dhamana ya asilimia 50 kwa wakopeshaji wa SME kwa mikopo mipya isiyolindwa itumike kwa mtaji wa kufanya kazi.

Serikali pia inatoa msamaha kutoka majukumu ya kukopesha uwajibikaji kwa wakopeshaji kutoa mikopo kwa wateja waliopo wa biashara ndogo.

Msamaha huu ni muda wa miezi sita na inatumika kwa madeni yoyote kwa madhumuni ya biashara, pamoja na mkopo mpya, ongezeko la kikomo cha mkopo na mabadiliko na marekebisho ya mkopo.

Kusaidia mikoa na sekta

Serikali imeweka kando $1 bilioni kusaidia jamii, mikoa na viwanda vilivyoathiriwa sana na mlipuko wa virus vya corona. Fedha hizi zitapatikana kusaidia wakati wa mlipuko na kusaidia na upatikanaji tena. Kwa kuongezea, Serikali inasaidia tasnia yetu ya ndege kupitia kifurushi cha hadi $715 milioni.

Hatua za muda za Mpango wa JobMaker ili kuzisaidia biashara

Kama sehemu ya Bajeti ya 2020–21, serikali inatekeleza hatua kadhaa za kusaidia biashara kupona kutoka athari ya janga la virusi vya korona (COVID-19).

Hatua hizi zinahusu kudai upungufu wa ushuru, vipunguzi, na upunguzi wa mali kwa kipindi cha ushuru. Zitasaidia biashara kupitia athari za kifedha za COVID-19 kwa miaka ya kifedha ya 2020–21 na 2021–22.

Hatua hizi zinafuata:

  • Mkopo wa Kuajira wa JobMaker
  • Gharama kamili wa muda
  • Hasara kurudi nyuma
  • Kuunga mkono uwekezaji – upunguzi thamani
  • Kufuta mali ya papo hapo
  • Kuongeza kizingiti cha mauzo ya vitu ya biashara ndogo